Al-Anbiyaa 21:72
الأنبياءوَوَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَـٰلِحِينَ
Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawafanya kuwa watu wema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia wawe watu wema. [72]
[72] Na tukampa Ibrahim mtoto Is-haq, na kutokana na Is-haq tukampa Yaaqubu, zaidi kuliko aliyo taka. Na wote wawili, Is-haq na Yaaqubu tuliwajaalia kuwa ni watu wema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Alimneemesha Ibrãhîm kwa kumtunuku Isḫâq alipomuomba, na zaidi ya hilo Alimtunuku, kutokana na Isḫâq, Ya‛qûb. Na kila mmoja kati ya Ibrãhîm na Isḫâq na Ya‛qûb Allah Mtukufu Alimjaalia kuwa mwema na mtiifu Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net