Al-Anbiyaa 21:71
الأنبياءوَنَجَّيْنَـٰهُ وَلُوطًا إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلَّتِى بَـٰرَكْنَا فِيهَا لِلْعَـٰلَمِينَ
Na tukamwokoa yeye na Luuti, tukawapeleka kwenye nchi tuliyoibariki kwa ajili ya walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenye nchi tulio ibariki kwa ajili ya walimwengu wote. [71]
[71] Na tukamwokoa yeye na Luut'i na njama zilizo pangwa, wakaelekea kwenye nchi tuliyo ijaalia kheri nyingi kwa watu wote, na tukawapeleka huko Manabii wengi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukamuokoa Ibrãhîm na Lûṭ ambaye alimuamini kutoka ‛Irâq na tukawatoa huko hadi Shâm ambako tulikubariki kwa kheri nyingi, na huko kulikuwa na Manabii, rehema na amani ziwashukie, wengi zaidi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net