Al-Anbiyaa 21:74
الأنبياءوَلُوطًا ءَاتَيْنَـٰهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَـٰهُ مِنَ ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِى كَانَت تَّعْمَلُ ٱلْخَبَـٰٓئِثَ ۗ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَـٰسِقِينَ
Na Lut tukampa hukumu na elimu na tukamwokoa kutokana na ule mji uliokuwa ukifanya machafu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa na ule mji ulio kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu. [74]
[74] Luut'i tukampa kauli ya kukata na madhubuti katika hukumu na ilimu yenye manufaa. Na tukamwokoa kutokana na mji ambao watu wake wanafanya kitendo cha namna ya peke yake katika uovu. Hakika hao walikuwa watu walio shikilia kufanya maovu, walio toka kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu na tabia iliyo zowewa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulimpa Lûṭ unabii, kufanya uamuzi baina ya watesi na ujuzi wa amri za Allah Mtukufu na Dini Yake. Na tulimuokoa na kijiji chake Sadûm ambacho watu wake walikuwa wakifanya mambo machafu. Wao, kwa sababu ya machafu na maovu ambayo watu wa uovu na uchafu walikua wakiyatenda, walikuwa nje ya utiifu wa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net