Al-Anbiyaa 21:7
الأنبياءوَمَآ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۖ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Na hatukuwatuma kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia ufunuo (wahyi). Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui. [7]
[7] Ewe Nabii! Kabla yako wewe hatukuwatumia watu ila watu wa kibinaadamu vile vile, ambao tuliwafunulia Dini waifikishe kwa watu. Basi, enyi mnao kataa! Waulizeni wanazuoni wajuao ilimu za Vitabu vilivyo teremka, ikiwa nyinyi hamyajui hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukuwatuma kabla yako, ewe Mtume, isipokuwa wanaume wa kibinadamu ambao tunawaletea wahyi, na hatukuwatuma Malaika. Basi waulizeni, enyi watu wa Makkah, wenye ujuzi wa vitabu vilivyoteremshwa huko nyuma iwapo hamjui hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net