Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 8

Al-Anbiyaa 21:8

الأنبياء

وَمَا جَعَلْنَـٰهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَمَا كَانُوا۟ خَـٰلِدِينَ

Maana

Wala hatukuwafanya miili isiyokula chakula, wala hawakuwa wenye kuishi milele.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hatukuwafanya miili isiyo kula chakula, wala hawakuwa wenye kuishi milele. [8]

[8] Wala Sisi hatukuwajaalia Mitume kuwa na miili inayo khitalifiana na miili ya wanaadamu wengine, wakawa wanaishi bila ya chakula, na wakabaki siku zote, na wala hawakuwa wanaishi daima milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hatukuwafanya wale Mitume kabla yako wawe nje ya tabia ya binadamu, wasihitaji chakula na kinywaji, na hawakuwa ni wenye kukaa milele wakawa hawafi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net