Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 6

Al-Anbiyaa 21:6

الأنبياء

مَآ ءَامَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَآ ۖ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ

Maana

Hawakuamini kabla yao watu wa mji wowote tuliouangamiza. Basi, je, hawa ndio wataamini?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hawakuamini kabla yao watu wa mji tulio uangamiza. Basi, je, wataamini hawa? [6]

[6] Hizo kaumu tulizo ziangamiza baada ya kukadhibisha hiyo miujiza hazikuamini. Basi, je! Watakuja amini hawa yatapo wajia hayo wayatakayo?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakuna mji wowote ulioamini kabla ya makafiri wa Makkah ambao watu wake walitaka miujiza kutoka kwa Mtume wao na ikatokea kweli, isipokua walikanusha na tukawaangamiza. Basi je, makafiri wa Makkah wataamini iwapo itatokea miujiza waliyoitaka? Sivyo, wao hawataamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net