Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 42

Al-Anbiyaa 21:42

الأنبياء

قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ مِنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ

Maana

Sema: Ni nani anayewalinda usiku na mchana mbali na Arrahmani (Mwingi wa rehema)? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Nani anaye kulindeni usiku na mchana na Arrahmani Mwingi wa Rehema? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi. [42]

[42] Ewe Nabii! Waambie: Ni nani anaye kuhifadhini na nakama zake wakati wa usiku na mchana, na akakurehemuni na kukuneemesheni? Hapana awezae hayo. Lakini wao wanaipuuza Qur'ani ambayo ndiyo inawakumbusha ya kuwafaa na kuwalinda na adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaoifanyia haraka adhabu, «Hakuna anayewahifadhi na kuwalinda na adhabu ya Allah Mtukufu ikiwashukia, usiku wenu au mchana wenu, katika kulala kwenu au kuwa macho kwenu?» Bali wao wamepumbaa na wameghafilika na Qur’ani na mawaidha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net