Al-Anbiyaa 21:41
الأنبياءوَلَقَدِ ٱسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُوا۟ مِنْهُم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Na Mitume walio kabla yako walikwishadhihakiwa. Kwa hivyo wale waliowafanyia masihara yaliwafika yale waliyokuwa wakiyafanyia dhihaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale walio wafanyia maskhara yaliwafika yale waliyo kuwa wakiyafanyia dhihaka. [41]
[41] Na Mitume wa kabla yako yaliwapata vile vile ya kufanyiwa kejeli na makafiri katika kaumu zao. Ikawateremkia hao walio wakataa Mitume na kuwafanyia maskhara adhabu hiyo hiyo ambayo wao waliifanyia maskhara na kejeli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mitume kabla yako, ewe Mtume, walifanyiwa shere, ikawafikia wale waliokuwa wakiifanyia shere adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia kejeli.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net