Al-Anbiyaa 21:40
الأنبياءبَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ
Bali itawafikia kwa ghafla, na itawashitua na wala hawataweza kuirudisha, wala hawatapewa muhula!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na wala hawataweza kuurudisha, wala hawatapewa muhula! [40]
[40] Kiyama hakiwajii kwa kukitarajia kutokea kwake, bali kitawazukia kwa ghafla tu kiwababaishe, wasiweze kukirudisha, wala wao hawatapewa muhula wa kutubia na kutafuta udhuru kwa waliyo kwisha yatenda..
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Kiyama kitawajia ghafla, hapo wataduwaa na watakuwa na hofu kubwa na hawataweza kuizuia adhabu isiwapate, na hawatapewa nafasi ya kutubia wala kutoa udhuru.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net