Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 4

Al-Anbiyaa 21:4

الأنبياء

قَالَ رَبِّى يَعْلَمُ ٱلْقَوْلَ فِى ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kujua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. [4]

[4] Mtume, kwa kuwa Mwenyezi Mungu kamjuulisha waliyo kuwa wakiyasema kwa siri, aliwaambia: Mola wangu Mlezi anayajua yote yanayo semwa katika mbingu na katika ardhi, na Yeye ndiye anaye sikia kila linalo sikiwa; na anajua kila linalo tokea..

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), analirudisha kila jambo kwa Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, anasema, «Mola wangu Analijua jambo la mbinguni na la ardhini na Anayajua maneno yenu mnayoyasema kwa siri, na Yeye Ndiye Mwenye kuyasikia maneno yenu, Ndiye Mwenye kuzijua hali zenu.» Katika haya pana onyo kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net