Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 3

Al-Anbiyaa 21:3

الأنبياء

لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا۟ ٱلنَّجْوَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ هَلْ هَـٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ ٱلسِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ

Maana

Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale waliodhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani huyu isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi! Je, mnauendea uchawi ilhali nyinyi mnaona?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi mnaona? [3]

[3] Nyoyo zao zimo katika pumbao, hazizingatii, wameshikilia kuficha njama zao za kumpinga Nabii na Qur'ani, wakiambizana wenyewe kwa wenyewe: Huyu Muhammad si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Na Mtume hawi ila Malaika. Basi, je! Mnamsadiki Muhammad na mnahudhuria baraza za uchawi na hali nyinyi mnaona kuwa hakika huo ni uchawi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nyoyo zao zimeghafilika na Qur’ani, zimeshughulika na ubatilifu wa dunia na matamanio yake, hawayafahamu yaliyomo ndani yake. Lakini madhalimu miongoni mwa Makureshi wamejikusanya pamoja juu ya jambo lililofichika, nalo ni kueneza yale ambayo kwayo wanawazuia watu kumuamini Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kuwa yeye ni binadamu mfano wao, hatafautiani na wao katika kitu chochote, na wanawaambia kwamba Qur’ani aliyoileta ni uchawi. (Wanawaambia kwa kusema) «Vipi mtakuja kwake na mumfuate na hali kwamba mnaona kwamba yeye ni binadamu kama nyinyi?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net