Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 35

Al-Anbiyaa 21:35

الأنبياء

كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ ٱلْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِٱلشَّرِّ وَٱلْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ

Maana

Kila nafsi itaonja mauti; na tunawajaribu kwa mtihani wa maovu na heri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa. [35]

[35] Kila nafsi haina budi kuonja mauti. Na Sisi tunakufanyieni hapa duniani kama wenye kukupeni mtihani, kwa kukupeni yenye manufaa yenu na yenye madhara pia, ili abagulike mwenye kushukuru kwa kupewa kheri na kuvumilia balaa, na yule asiye na fadhila kwa neema aipatayo na anapapatika akipata misiba. Nanyi mtarejeshwa kwetu, na hapo tutakuhisabieni vitendo vyenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila nafsi ni yenye kuonja kifo hapana budi namna utakavyorefuka umri wake duniani. Na kuweko kwake maishani hakukuwa isipokuwa ni mtihani wa majukumu ya maamrisho na makatazo na mabadiliko ya hali, mazuri na mabaya, kisha baada ya hapo kuna kurudi na kurejea kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, ili kuhesabiwa na kulipwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net