Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 36

Al-Anbiyaa 21:36

الأنبياء

وَإِذَا رَءَاكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا ٱلَّذِى يَذْكُرُ ءَالِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ ٱلرَّحْمَـٰنِ هُمْ كَـٰفِرُونَ

Maana

Na wanapokuona wale waliokufuru, hawakufanyi wewe isipokuwa ni kitu cha masihara tu, (wakisema): Je, huyu ndiye anayeitaja miungu yenu? Na hali wao wanakufuru kumkumbuka Arrahman (Mwingi wa rehema)!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakikuona walio kufuru hawakufanyi wewe ila ni kitu cha maskhara tu, (wakisema): Je! Ndiye huyu anaye itaja miungu yenu? Na hali wao wanakataa kumkumbuka Arrahman, Mwingi wa Rehema! [36]

[36] Na wakikuona, ewe Nabii, wale walio mkataa Mwenyezi Mungu na ulio kuja nayo wewe, hawakufanyii wewe ila maskhara na kejeli. Huambiana wao kwa wao: Ndiye huyu anaye watia aibu miungu yenu? Na hali wao hawasadiki kumdhukuru Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliye waeneza rehema yake!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri wanapokuona, ewe Mtume, wanakuashiria kwa kukufanyia shere, huwa wakiambiana wao kwa wao, «Je, ni huyu yule mtu anayewatukana waungu wenu?» Wao wamemkanusha Mwingi wa rehema na wamezikanusha neema Zake na yale Aliyoyateremsha ya Qur’ani na uongofu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net