Al-Anbiyaa 21:34
الأنبياءوَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ ٱلْخُلْدَ ۖ أَفَإِي۟ن مِّتَّ فَهُمُ ٱلْخَـٰلِدُونَ
Nasi hatukumfanya mwanadamu yeyote kabla yako kuwa na uhai wa milele. Basi je, ukifa wewe, wao wataishi milele?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele. Basi je! Ukifa wewe, wao wataishi milele? [34]
[34] Ewe Nabii! Hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako wewe aishi milele, hata ikawa hao makafiri wakawa wanakutamania ufe wewe. Vipi wanakutamania mauti wewe na hali na wao vile vile watakufa kama wewe? Ukifa wewe, je, ndio wao watabakia kushinda wanaadamu wote?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hatukumfanya mwadamu yoyote kabla yako, ewe Mtume, asalie duniani milele. Basi ufapo wewe, kwani wao wana matumaini ya kuishi daima baada yako? Hili haliwi. Katika aya hii pana dalili kwamba Al-Khadir, amani imshukie, ameshakufa, kwa kuwa yeye ni mwanadamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net