Al-Anbiyaa 21:33
الأنبياءوَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
Na Yeye ndiye aliyeumba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea. [33]
[33] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba usiku na mchana, na jua na mwezi. Vyote hivyo vinakwenda katika njia zake kama alivyo zijaalia Mwenyezi Mungu, na zinamtakasa bila ya kupotea. Maoni ya wataalamu juu ya Aya 33: "Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea." Kila sayari ya mbinguni ina mzunguko wake makhsusi inayo ogelea kuufuata. Na zote hizo hazisiti, na zinakwenda kwa mwendo wao maalumu katika anga. Na sisi tunaona hayo kwa hakika kwa kutazama mwendo wa jua na mwezi. Kama kadhaalika mzunguko wa ardhi wake wenyewe ndio unao leta usiku na mchana kwa zamu, kama kwamba unaogelea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Aliyeumba usiku ili watu wapate kutulia, na mchana ili wapate kutafuta maisha. Na Ameumba jua, likiwa ni alama ya mchana, na mwezi, ukiwa ni alama ya usiku. Na kila kimojawapo ya hivyo viwili kina njia ya kupitia na kuogelea hakiendi kando nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net