Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 18

Al-Anbiyaa 21:18

الأنبياء

بَلْ نَقْذِفُ بِٱلْحَقِّ عَلَى ٱلْبَـٰطِلِ فَيَدْمَغُهُۥ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ ٱلْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ

Maana

Bali tunaitupa haki juu ya batili, ikaivunja na mara ikatoweka. Na ole wenu kwa mnayoyazua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua. [18]

[18] Lakini jambo linalo tuelekea Sisi kulifanya ni kuipambanisha kweli juu ya uwongo ipate kuuondoa. Na nyinyi makafiri mtahiliki kwa sababu ya kumzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Bali tunaisukuma haki na tunaifafanua, na hapo urongo unaporomoka, na punde si punde unaondoka na kupotea. Na nyinyi, enyi washirikina, mtapata adhabu huko Akhera kwa kumsifu kwenu Mola wenu kwa sifa zisizonasibiana na Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net