Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sura ya 21

Al-Anbiyaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 18

بَلْ نَقْذِفُ بِٱلْحَقِّ عَلَى ٱلْبَـٰطِلِ فَيَدْمَغُهُۥ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ ٱلْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ 18

{18} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba alichukua dhamana na ya kuihakikisha haki na kuibatilisha batili, hata ikiwa ni batili iliyosemwa na kujadiliwa. Basi Mwenyezi Mungu huteremsha haki, elimu, na ubainisho wenye kuivunja ikapotea, kwa hivyo ukambainikia kila mtu ubatili wake, "mara ikatoweka." Na hili ni la jumla katika masuala yote ya kidini. Mwenye batili yeyote hawezi kuleta fikira potovu ya kiakili wala ya kimaandiko katika kuisimamisha batili au kuikataa, isipokuwa katika ushahidi wa Mwenyezi Mungu, kuna mambo ya uhakika ya kiakili na ya kimaandiko yenye kuyaiondoa na kuikomesha kauli hiyo batili. Basi ubatili wake mara unambainikia kila mmoja. Na hili linabainika kwa kuyarejelea masuala moja baada ya jingine, na utayapata yako vivyo hivyo. Kisha akasema: Nanyi enyi mnaomuelezea Mwenyezi Mungu kwa maelezo yasiyomfailia, kama vile kujifanyia mwana na mke na kwamba ana wenza na washirika mna fungu lenu na mgao wenu katika hayo, ambao kwa huo mtapata adhabu, majuto na hasara. Na hamna faida yoyote katika yale mliyoyasema wala hayawarudii kwa lolote la kuwapa matumaini, wala la kufanya matendo kwa ajili yake, na kufanya bidii kulifikia isipokuwa kinyume cha makusudio yenu, ambayo ni kuambulia patupu na kunyimwa.