Al-Anbiyaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَلَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُۥ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِۦ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ 19
{19} Kisha akajulisha kwamba ni wake ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake. Vyote ni waja wake na wamilikiwa wake. Na hakuna hata mmoja wao aliye na ufalme wala fungu katika ufalme huo wala hata kumsaidia juu yake, na wala hawezi yeyote kufanya uombezi isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi miungu inawezaje kuchukuliwa katika hawa? Na Mwenyezi Mungu anawezaje kufanyiwa mwana kutoka kwa hawa? Kwa hivyo ametukuka na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mfalme Mkuu ambaye zimemnyenyekea Yeye shingo zote, na yakadhalilika kwake magumu yote, na wamemhofu malaika wote waliokaribu zaidi naye, na wote wanamtii kwa kumuabudu kwa ibada za kuendelea daima. Na ndiyo maana akasema, "Na wale walioko kwake" [kama vile] malaika, "hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki;" kwa sababu ya utashi wao mkubwa, na ukamilifu wa upendo wao, na nguvu za miili yao.