Al-Anbiyaa 21:17
الأنبياءلَوْ أَرَدْنَآ أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّٱتَّخَذْنَـٰهُ مِن لَّدُنَّآ إِن كُنَّا فَـٰعِلِينَ
Kama tungelitaka kufanya pumbao, tungejifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungelikuwa ni wafanyao hivyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungeli kuwa ni wafanyao mchezo. [17]
[17] Lau kuwa tunataka kufanya mchezo na pumbao isingeli mkinika kuchukua ila yaliyo katika ufalme wetu, kwani hapana ufalme ila wetu - ingeli kuwa Sisi ni wa kufanya hayo. Wala nasi si wenye kufanya hayo, kwa kuwa si laiki ya haki yetu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lau tungetaka kujifanyia kipumbazi cha mtoto au mke tungalikifanya kutoka kwetu, na sio kwenu. Hatukuwa ni wenye kufanya hilo kwa kuwa ni muhali kwetu kuwa na mtoto au mke.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net