Al-Anbiyaa 21:14
الأنبياءقَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ
Wakasema: "Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhaalimu. [14]
[14] Kwa kuwa hao makafiri wamekwisha sikia wanavyo kejeliwa na wanavyo itwa kwenda teketezwa na wana yakini nako, basi watasema: Hakika kweli sisi tulikuwa ni wenye kudhulumu tulipo yaacha yanayo tunafiisha, na tusiziamini Ishara za Mola wetu Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawakuwa na majibu yoyote isipokuwa ni kukubali makosa yao na kusema, «Ee maangamivu yetu! Tumejidhulumu nafsi zetu kwa ukafiri wetu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net