Al-Anbiyaa 21:13
الأنبياءلَا تَرْكُضُوا۟ وَٱرْجِعُوٓا۟ إِلَىٰ مَآ أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَـٰكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْـَٔلُونَ
Msikimbie! Na rejeeni kwenye yale yale mliyostareheshwa kwayo, na maskani zenu, ili mpate kuulizwa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Msikimbie! Na rejeeni kwenye zile zile starehe zenu, na maskani zenu, mpate kusailiwa! [13]
[13] Enyi wapinzani! Msikimbie! Hapana kitu chochote kitacho kulindeni na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Rudini kwenye zile zile neema na majumba mliyo kuwa nayo, huenda watumishi wenu na wenzenu watakutakeni msaada na rai kama ilivyo kuwa ada yenu. Wapi! Hamtoweza!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakaitwa wakiwa katika hali hii na kuambiwa, «Msikimbie, na rudini kwenye ladha zenu na starehe zenu katika ulimwengu wenu wenye kupumbaza na nyumba zenu zilizojengwa, kwani huenda mkaulizwa jambo kuhusu ulimwengu wenu. Na hiyo ni kwa njia ya kuwafanyia shere na ubishi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net