Al-Anbiyaa 21:15
الأنبياءفَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَىٰهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَـٰهُمْ حَصِيدًا خَـٰمِدِينَ
Basi hakikuacha hicho kuwa ndicho kilio chao mpaka tukawafanya kama waliofyekwa, wamezimika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakikuacha hicho kuwa kilio chao mpaka tukawafanya kama walio fyekwa, wamezimika. [15]
[15] Maneno hayo hawaachi kuyakariri na kuyapigia makelele mpaka kwa adhabu yetu tukawafanya kama mimea iliyo fyekwa, na moto ulio zimika, hawana tena uhai.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yaliendelea maneno hayo – nayo ni yale ya kujiapiza wenyewe maangamivu na kukubali kuwa wamejidhulumu wenyewe- kuwa ndiyo mwito wao wanaoukariri mpaka tukawafanya kama mimea ya mazao iliyovunwa, wakiwa wametulia hawana uhai. Basi kuweni na hadhari, enyi mnaoambiwa, na kuendelea kumkanusha Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), yasije yakawashukia nyinyi yale yaliyowashukia watu waliopita kabla yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net