Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 99

Al-Baqara 2:99

البقرة

وَلَقَدْ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَآ إِلَّا ٱلْفَـٰسِقُونَ

Maana

Hakika tumekuteremshia ishara zilizo wazi na hapana anayezikufuru isipokuwa wenye kupindukia mipaka (wapotovu).

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika tumekuteremshia Ishara zilizo wazi na hapana wanao zikataa ila wapotovu. [99]

[99] Na Jibril hateremshi kwenye moyo wako kila Ishara na hoja zilizo wazi, ambazo haiwezekani kwa mwenye kutafuta haki kikweli ila aziamini tu. Na hapana mwenye kuzikataa Ishara kama hizo ila wale wafanyao inda na inadi, ambao wametokana na mwenendo wa maumbile walio umbwa nao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tulikuteremshia aya zilizo wazi, zinazoonyesha kuwa wewe ni Mtume wa Allah Mtukufu kikweli; na hawazikanushi aya hizo isipokuwa wenye kutoka nje ya Dini ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net