Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 98

Al-Baqara 2:98

البقرة

مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوٌّ لِّلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Aliyekuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri. [98]

[98] Basi yeyote anaye kuwa ni adui wa Jibril, au Mikail, au Malaika yeyote au Mtume yeyote, miongoni mwa Malaika na Mitume wa Mwenyezi Mungu, ambao hawafanyi kitu wala hawapeleki ujumbe ila kama vile Mwenyezi Mungu anavyo waamrisha, basi mtu huyo anakuwa ni adui wa Mwenyezi Mungu, na anakuwa kafiri anamkataa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kumfanyia uadui Allah Mtukufu, Malaika Wake, Wajumbe Wake ambao ni Malaika au binadamu, hasahasa Malaika wawili: Jibrili na Mikaili, huwa amemfanyia uadui Allah Mtukufu. Sababu Mayahudi walidai kwamba Jibrili ni adui wao na Mikaili ni rafiki yao. Allah Mtukufu Akawajulisha kwamba mwenye kuwa adui wa mmoja katika wao huwa ni adui wa Mwengine na pia ni adui wa Allah Mtukufu. Kwani Allah Mtukufu ni adui wa wenye kuyakanusha yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake Muhammad, rehema na amani zimshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net