Al-Baqara 2:97
البقرةقُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ
Sema: Aliyekuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliyeiteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayothibitisha yaliyokuwa kabla yake, na ni uongofu na bishara njema kwa Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini. [97]
[97] Na baadhi yao wanadai kuwa wanakupinga na wanakikataa Kitabu chako kwa kuwa ati wao ni maadui wa Jibril anaye kufikishia hichi Kitabu. Basi sema ewe Nabii uwaambie: Anaye kuwa Jibril ni adui wake, basi vile vile huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu Jibril haji na Kitabu hichi kwa nafsi yake, bali anakiteremsha kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na Kitabu hichi kinathibitisha Vitabu vilivyo tangulia kutoka mbinguni.. na kinathibitisha Kitabu chenu wenyewe..na hii Qur'ani (inayo teremshwa na Jibril kutoka kwa Mwenyezi Mungu) ni Uwongofu na Bishara njema kwa Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia Mayahudi waliposema, “Jibrili ni adui yetu miongoni mwa Malaika.”: “Mwenye kuwa ni adui wa Jibrili, basi ajue kuwa yeye ameiteremsha Qur’ani na kuitia ndani ya moyo wako kwa idhini ya Allah Mtukufu, ikiwa ni yenye kuvisadikisha vitabu vya Allah Mtukufu vilivyoitangulia, yenye kuongoza kwenye njia ya haki na yenye kuwapa wenye kuamini bishara ya kila wema wa dunia na Akhera.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net