Al-Baqara 2:96
البقرةوَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ ٱلنَّاسِ عَلَىٰ حَيَوٰةٍ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِۦ مِنَ ٱلْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِمَا يَعْمَلُونَ
Na hakika utawapata ni wenye pupa ya kuishi kuwashinda watu wote, na kuliko washirikina. Mmoja wao anatamani lau angelipewa umri wa miaka elfu. Wala hilo (la kuzidishiwa umri) haliwezi kumweka mbali na adhabu, ili apewe umri mrefu. Na Mwenyezi Mungu anayaona vyema wanayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu wote kwa pupa ya kuishi, na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anatamani lau angeli pewa umri wa miaka elfu. Wala hayo ya kuzidishiwa umri hayamuondoshei adhabu; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda. [96]
[96] Bila ya shaka yoyote utawakuta wao ndio wamewashinda watu wote kwa pupa waliyo nayo kuwania maisha ya dunia ya kila namna, ya utukufu na unyonge. Na hiyo pupa yao inashinda ya makafiri washirikina (mapagani) wasio amini kufufuliwa wala Pepo. Kwa hivyo wanapenda lau kuwa wangelizidishiwa umri wakaishi hata miaka elfu. Na hata wangeliishi vipi hawawezi kuepuka adhabu ya Mwenyezi Mungu inayo wangojea. Kwani Yeye ni Mjuzi wa hao madhaalimu, na atawaonjesha malipo ya vitendo vyao wanavyo vitenda
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na utajua tena utajua, ewe Mtume, kuwa Mayahudi ni wenye kupenda mno, miongoni mwa watu, maisha marefu, hata yawe ni maisha ya unyonge na udhalilifu namna gani. Kupenda kwao maisha marefu kunazidi vile washirikina wanavyoyapenda. Myahudi anatamani lau ataishi miaka elfu moja. Na umri huo, lau aufikia, hautamwepusha na adhabu ya Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu, hakuna kitu chochote chenye kufichika Kwake katika matendo yao, na Atawalipa, kwa hiyo matendo yao, adhabu wanayostahiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net