Al-Baqara 2:95
البقرةوَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًۢا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ
Wala hawatayatamani kamwe; kwa sababu ya yale mikono yao ilitanguliza. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwajua vyema wanaodhulumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale yaliyo tangulizwa na mikono yao; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwajua vyema wanao dhulumu. [95]
[95] Lakini kwa hakika mambo yalivyo, wao hawayatamani mauti kabisa kwa dhulma walio ifanya, ambayo haifichikani kwa Mwenyezi Mungu. Yeye anawajua kuwa wao ni waongo kwa hayo wanao dai. Neema za Siku ya Kiyama zitakuwa ni za wachamngu, si za wafanyao maovu kama wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawatalifanya hilo kabisa, kwa wanayoyajua ya ukweli wa Nabii Muhammad, rehema na amani zimshukie, na ya urongo na uzushi wao, na kwa ukafiri na uasi walioufanya unaopelekea kukoseshwa Pepo na kuingia Motoni. Na Allah Mtukufu Anawajua madhalimu miongoni mwa waja wake na Atawalipa kwa dhulma zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net