Al-Baqara 2:100
البقرةأَوَكُلَّمَا عَـٰهَدُوا۟ عَهْدًا نَّبَذَهُۥ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Kwani kila wanapofunga agano, huwapo kikundi miongoni mwao kinalivunja? Bali wengi wao hawaamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini. [100]
[100] Na kama (hawa Wana wa Israili) walivyo kuwa vigeugeu katika itikadi na imani, hali kadhaalika walikuwa vigeugeu katika ahadi na mapatano wanayo choka nayo. Walikuwa kila wanapo fungamana na Waislamu au wengineo kwa maagano hutokea kikundi miongoni mwao wakavunjilia mbali maagano hayo. Kwani wengi wao hawaamini utukufu wa ahadi na utakatifu wa maagano.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni ubaya ulioje wa hali ya Wana wa Isrãîl katika kuvunja kwao ahadi! Kila wanapotoa ahadi, kinatoka kikundi cha watu katika wao wakaitupa na wakaivunja. Utawaona wanaifunga ahadi leo na kuitengua kesho. Bali wengi wao hawayaamini aliyokuja nayo Nabii wa Allah Mtukufu na Mtume wake Muhammad, rehema na amani Zimshukie yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net