Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 92

Al-Baqara 2:92

البقرة

وَلَقَدْ جَآءَكُم مُّوسَىٰ بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ثُمَّ ٱتَّخَذْتُمُ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِهِۦ وَأَنتُمْ ظَـٰلِمُونَ

Maana

Na alikujieni Musa na hoja zilizo wazi, kisha mkamchukua ndama (kumuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alikufikieni Musa na hoja zilizo waziwazi, kisha mkamchukua ndama (kumuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu. [92]

[92] Bali hakika nyinyi Mayahudi mlikanusha kwa uwazi Vitabu vyenu, na mkarejea katika ushirikina katika zama za Musa mwenyewe. Kwani Musa alikujieni na hoja zilizo wazi, na miujiza inayo hakikisha ukweli wake, lakini kiasi ya kukupeni mgongo tu alipo kwenda kusema na Mola wake Mlezi nyinyi mkaingia kuabudu ndama, na mkarajea katika ukafiri wenu wa kuabudu masanamu, na nyinyi mkawa mlio dhulumu mlio potea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Nabii wa Allah Mtukufu, Mûsã, aliwajia nyinyi na miujiza iliyo wazi yenye dalili ya ukweli wake, kama mafuriko, nzige, chawa, vyura na mengineyo katika yale aliyoyataja Allah Mtukufu katika Qur’ani tukufu. Pamoja na hivyo, mumemchukuwa ndama mkamfanya ni muabudiwa, baada ya Mûsã kuondoka kuenda kukutana na Mola wake. Na nyinyi kwa kufanya hivyo mnavuka mipaka ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net