Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 91

Al-Baqara 2:91

البقرة

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ ءَامِنُوا۟ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُوا۟ نُؤْمِنُ بِمَآ أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَآءَهُۥ وَهُوَ ٱلْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنۢبِيَآءَ ٱللَّهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Na wanapoambiwa: Yaaminini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Wao husema: 'Tunaamini tuliyoteremshiwa sisi.' Na huyakataa yasiyokuwa hayo. Na hali ya kuwa hii ndiyo haki inayothibitisha yale waliyo nayo wao. Sema: Mbona mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu hapo zamani ikiwa kweli mlikuwa Waumini?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Wao husema: Tunaamini tuliyo teremshiwa sisi. Na huyakataa yasiyo kuwa hayo. Na hali ya kuwa hii ndiyo Haki inayo thibitisha yale waliyo nayo wao. Sema: Mbona mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu hapo zamani ikiwa kweli mlikuwa Waumini? [91]

[91] Hizi ndizo dhamiri walizo nazo ndani ya nafsi zao. Lakini mbele za watu wakijitetea kuwa wao hawaiamini Qur'ani wanapo takiwa waamini, kwa kuwa wao hawaamini ila yale walio teremshiwa wao tu, na wanayakataa mengineyo. Na hakika wanasema uwongo kwa hayo madai yao kuwa wanaamini yaliyomo katika Taurati, kwani kwa kukitaa Kitabu hichi cha Qur'ani kinacho thibitisha Kitabu chao, ndio kuwa maana yake wanakataa Kitabu chao chenyewe, na kwa kuwa wao waliwauwa Manabii walio kuwa wanawaitia yale walio teremshiwa. Na wao kuwauwa hao ni dalili ya kukata kuwa hawauamini Ujumbe wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na baadhi ya Waislamu wanaposema kuwaambia Mayahudi, “Aminini Qur’ani,” wanasema, “Sisi tunaviamini vilivyoteremshwa kwa Mitume wetu.” Na wao wanakanusha vilivyoteremshwa na Allah Mtukufu baada yake, pamoja na kuwa ndio haki inayosadikisha vile walivyonavyo. Lau wao wangekua wanaviamini vitabu vyao kikweli, wangaliiamini Qur’ani iliyozisadikisha. Waambie, ewe Mtume, “Iwapo nyinyi mnayaamini yale mliyoteremshiwa na Allah Mtukufu kwenu, kwa nini mliwaua Manabii wa Allah Mtukufu wakati wa nyuma?”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net