Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 90

Al-Baqara 2:90

البقرة

بِئْسَمَا ٱشْتَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا۟ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۖ فَبَآءُو بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ

Maana

Kiovu kweli walichoziuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya kuona haya kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa waja wake. Basi wamejiletea wenyewe ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata mateso ya kudhalilisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kiovu kweli walicho jiuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kuona maya kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa waja wake. Basi wamejiletea wenyewe ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata mateso ya kudhalilisha. [90]

[90] Kiovu mno walicho ziuzia nafsi zao na roho zao! Na hayo ni kwa udhalimu wao, na kuona maya na kufanya uadui tu. Matamanio yao na chuki zao za kikabila, na ugozi walio nao, ndio ulio wapelekea kukataa tulio yateremsha Sisi, kwa kuonea uchungu vipi Mwenyezi Mungu kumpa ujumbe wake Mtume asiye tokana na wao. Wanamkatalia Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kukhiari atakavyo nani wa kumteremshia fadhila yake miongoni mwa waja wake. Kwa hivyo wamejipalilia wenyewe ghadhabu juu ya ghadhabu kwa kufuru zao na inadi zao na uhasidi wao. Na makafiri kama hawa watapata adhabu ya kuwadhalilisha na kutia uchungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni baya chaguo la Wana wa Isrãîl walilojichagulia. Kwani walibadilisha imani kwa ukafiri, (kwa kuacha imani na kuchukua ukafiri) kwa dhulma na uhasidi kwa kuwa Allah Mtukufu, kwa fadhila Zake, Alimteremshia Nabii Wake na Mtume Wake Muhammad, rehema na amani zimshukie. Basi wakarudi na hali ya kuwa Allah Mtukufu Ana ghadhabu juu yao kwa kumkanusha kwao Nabii Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, baada ya kuwa na ghadhabu juu yao kwa kuipotoa Taurati. Na wenye kukanusha unabii wa Muhammad, rehema na amani zimshukie, wana adhabu yenye kuwadhalilisha na kuwafanya wanyonge.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net