Al-Baqara 2:89
البقرةوَلَمَّا جَآءَهُمْ كِتَـٰبٌ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا۟ مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَلَمَّا جَآءَهُم مَّا عَرَفُوا۟ كَفَرُوا۟ بِهِۦ ۚ فَلَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ
Na kilipowajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinachothibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakiomba ushindi kuwashinda makafiri - yalipowajia yale waliyokuwa wakiyajua, waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya makafiri!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao! [89]
[89] Na Mtume wetu alipo wajia na Qur'ani, nayo ni Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha Taurati walio teremshiwa wao, na wakajua kutokana na hiyo Taurati ukweli uliomo katika Kitabu hichi (Qur'ani) walikataa kwa inadi na uhasidi tu, kwa sababu yamekuja hayo kutokana na Mtume asiye kuwa wa taifa lao la Wana wa Israili, juu ya kuwa kabla yake walipo kuwa wakipambana na makafiri washirikina ikiwa mpambano wa vita au majadiliano, wakitaja kuwa Mwenyezi Mungu atakuja wanusuru wao kwa kumtuma Nabii wa mwisho aliye bashiriwa katika Kitabu chao, na ambaye sifa zake zimewafikiana kabisa moja kwa moja na sifa za Muhammad. Jueni basi laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya watu wa namna hii wenye inda na ukanushi. (Mwenyezi Mungu alimwambia Musa: "Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe...mtu asiye sikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake." --Kumbukumbu la Torati 18.18-22. Maana ya haya ni: Taurati inasema kwamba Nabii Musa aliambiwa na Mungu kwamba atawaletea Nabii kutokana na ndugu za Wana wa Israili, yaani Waarabu. Na asiye mfuata Nabii huyo Mwenyezi Mungu atamuadhibu.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ilipowajia Qur’ani inayotoka kwa Allah Mtukufu, ikisadikisha yale ambayo waliokuwa nayo kwenye Taurati, waliikanusha na kuukataa utume wa Muhammad, sala na salamu zimshukie. Na walikuwa, kabla ya kutumilizwa kwake, wakitumai kusaidiwa na yeye dhidi ya washirikina wa Kiarabu, na walikuwa wakisema, “Umekaribia wakati wa kutumilizwa Mtume wa zama za mwisho ambaye sisi tutamfuata na tutapigana na nyinyi tukiwa pamoja na yeye.” Alipowajia huyo Mtume, ambaye walizijua sifa zake na ukweli wake, walimkataa na walimkanusha. Basi laana ya Allah Mtukufu imshukie kila aliyemkanusha Nabii na Mtume wa Allah Mtukufu Muhammad, rehema na amani zimshukie, na kukanusha Kitabu chake ambacho Allah Mtukufu alimletea kwa njia ya Wahyi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net