Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 88

Al-Baqara 2:88

البقرة

وَقَالُوا۟ قُلُوبُنَا غُلْفٌۢ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ

Maana

Na walisema: 'Nyoyo zetu zimefunikwa.' Bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao; kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walisema: Nyoyo zetu zimefunikwa. Bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao: kwa hivyo ni kidogo tu wanayo yaamini. [88]

[88] Hali kadhaalika msimamo wenu kwa Mtume wetu Muhammad, Nabii wa mwisho. Mlimwambia alipo kuiteni msilimu: Nyoyo zetu zimefunikwa kwa vifuniko visivyo achilia kupenya huo wito wako. Basi sisi hatuelewi kitu chochote unacho sema! Wala nyoyo zao hazikufunikwa kama wanavyo dai, lakini wamepanda kiburi tu, na wakakhiari upotovu kuliko uwongofu. Basi Mwenyezi Mungu amewalaani kwa ukafiri wao, na amedhoofisha yakini yao na imani yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wana wa Isrãîl walisema kumwambia Nabii na Mtume wa Allah Mtukufu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, “Nyoyo zetu zimezibwa kwa namna ambayo maneno yako hayapenyezi ndani yake.” Mambo si kama walivyodai. Bali nyonyo zao zimelaaniwa, zimepigwa muhuri juu ya hiyo laana. Na wao wamefukuzwa kutoka kwenye rehema za Allah Mtukufu kwa sababu ya kukanusha kwao. Wao hawaamini isipokuwa imani chache isiyowafaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net