Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 93

Al-Baqara 2:93

البقرة

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُوا۟ مَآ ءَاتَيْنَـٰكُم بِقُوَّةٍ وَٱسْمَعُوا۟ ۖ قَالُوا۟ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا۟ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِۦٓ إِيمَـٰنُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Na tulipochukua agano lenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya tuliyokupeni na sikieni. Wakasema: 'Tumesikia na tumeasi!' Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa kufuru yao. Sema: Ni uovu mno iliyokuamrisheni imani yenu ikiwa nyinyi ni waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulipo chukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya tuliyo kupeni na sikieni. Wakasema: Tumesikia na tumekataa! Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa kufuru yao. Sema: Ni uovu mno iliyo kuamrisheni imani yenu ikiwa ni wenye kuamini. [93]

[93] Na alipo kuleteeni Taurati mkaziona amri ngumu ziliomo ndani yake, mkaona mizito mizigo yake na mkaitilia shaka, Mwenyezi Mungu alikuonyesheni Ishara ya ukweli wa Kitabu hicho na faida ya mafunzo yake kwenu. Akaunyanyua Mlima wa T'uur juu ya vichwa vyenu hata ukawa kama kiwingu, na mkadhani kuwa utakuangukieni. Hapo mkaonyesha kukubali na kut'ii. Tukachukua ahadi yenu kuwa hamtaghurika na pumbao katika kufuata yaliyomo katika Kitabu hichi. Mkasema: Tumeamini na tumesikia. Lakini vitendo vyenu vimefichua uasi wenu, na kwamba imani haijaingia katika nyoyo zenu. Wala hayumkini kuwa imani imeingia katika nyoyo za watu walio shughulishwa na mapenzi ya kumuabudu ndama. Imani yenu hiyo mnayo dai basi imekusozeni kwenye maovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni, wakati tulipochukua kwenu ahadi yenye mkazo ya kuikubali Taurati aliyokuja nayo Mûsã, mkavunja ahadi, tukaliinua jabali la Ṭūr juu ya vichwa vyenu na tukasema, “Chukueni tulichowapa kwa bidii, na msikie na mtii, au tutaliangusha jabali juu yenu.” Mkasema, “Tumesikia kauli yako na tumeasi amri yako,” kwa kuwa ibada ya ndama imetangamana na nyoyo zenu kwa sababu ya kuendelea kwenu sana kwenye ukafiri. Waambie, ewe Mtume, Ni mbaya iliyoje hiyo njia ya ukafiri na upotevu ambayo imani yenu imewapeleka, iwapo nyinyi mnayasadiki yale yaliyoteremshwa kwenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net