Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 82

Al-Baqara 2:82

البقرة

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Na wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio watu wa Bustanini, humo watadumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio amini na wakatenda mema, hao ndio watu wa Peponi, humo watadumu. [82]

[82] Na wale walio amini na wakatenda mema hao ndio watu wa Peponi, kwa sababu wao wameamini na wakatimiza iliyo wajibisha Imani yao, nayo ni vitendo vyema, basi wao watakaa Peponi daima milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hukumu ya Allah Mtukufu iliyothibiti, kwa upande mwengine, ni kwamba wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake imani ya kikweli iliyosafika na Wakafanya vitendo vinavyoambatana na Sheria ya Allah Mtukufu Aliyowapelekea Mitume Wake kwa njia ya Wahyi, hao watakaa Peponi makao ya milele yasiyokatika huko Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net