Al-Baqara 2:83
البقرةوَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَقُولُوا۟ لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ
Na tulipofunga agano na Wana wa Israili: 'Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na semeni na watu kwa wema, na shikeni Sala, na toeni Zaka.' Kisha mkageuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tulipo funga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na semeni na watu kwa wema, na shikeni Swala, na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipo kuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza. [83]
[83] Mbali na haya yote, nyinyi jamaa wa Kiyahudi, mnaendelea kuyashughulikia madhambi na kuvunja ahadi, na kupindukia mipaka aliyo kuwekeeni Mwenyezi Mungu. Kumbukeni tulipo chukua ahadi kwenu katika Taurat kuwa hamtamuabudu ila Mwenyezi Mungu, na mwatendee wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na mnapo zungumza na watu mtumie maneno mazuri ya kuleta masikilizano baina yenu nao wala sio ya kukutenganisheni, na mtimize yaliyo kuwa waajibu juu yenu, nayo ni Swala, na Zaka. Na kumbukeni ulikuwaje mwendo wenu katika ahadi hiyo? Vipi mlivyo ivunja na mkajipuuza nao, isipo kuwa wachache tu ndio walio ifuata Haki?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Kumbukeni, enyi Wana wa Isrãîl, tulipochukua ahadi ya mkazo kwenu kwamba mtamuabudu Allah Mtukufu peke Yake Asiye na mshirika, muwafanyie wema wazazi wawili na watoto waliofiliwa na baba zao nao wako chini ya umri wa kubaleghe na masikini na kwamba muwaambie watu maneno mazuri, pamoja na kusimamisha Swala na kutoa Zaka. Kisha mkageuka na mkavunja ahadi, isipokuwa wachache katika nyinyi waliosimama imara juu yake. Na nyinyi bado mnaendelea kugeuka kwenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net