Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 81

Al-Baqara 2:81

البقرة

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَـٰطَتْ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Ndiyo, anayechuma ubaya - na makosa yake yakamzingira, hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naam, anaye chuma ubaya - na makosa yake yakamzunguka hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu. [81]

[81] Ukweli wa mambo ni kuwa nyinyi mnamzulia Mwenyezi Mungu uwongo. Kwani hukumu ya Mwenyezi Mungu inapitishwa kwa viumbe vyake vyote sawa sawa, hapana farka baina ya Yuhudi na asiye kuwa Yahudi. Wenye kutenda maovu, na maovu yakawazunguka hao waovu mpaka njia za kuokoka zote zikazibwa, basi hao ndio watu wa Motoni na huko watudumu milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hukumu ya Allah Mtukufu imethibiti kwamba mwenye kutenda makosa mpaka yakamtia ukafirini na madhambi yake yakamtawala yeye sehemu zake zote, na hali hii haiwi isipokuwa kwa mwenye kumshirikisha Allah Mtukufu, wote hao, washirikina na makafiri, ndio wenye kukaa Motoni makao ya milele yasiyokatika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net