Al-Baqara 2:80
البقرةوَقَالُوا۟ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ ٱللَّهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ ٱللَّهُ عَهْدَهُۥٓ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Na walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema: Mmechukua agano kwa Mwenyezi Mungu? Kwa hivyo Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na agano lake. Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema: Mmechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu? Kweli Mwenyezi Mungu hatokwenda kinyume na ahadi yake. Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyo yajua? [80]
[80] Na katika khitilafu zao ni haya wanayo yapata kwa makohani ya kuwa Moto hautawagusa Mayahudi hata wakifanya maasia namna gani ila kwa muda wa siku chache tu. Basi waambie ewe Muhammad!: Nyinyi mmeagana na Mwenyezi Mungu kwa hayo, hata mkawa mmetumaini kuwa Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake, au mnamzulia uwongo tu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walisema Wana wa Isrãîl, “Moto hautupati huko Akhera isipokuwa kwa siku chache zinazohesabika.” Waambie, ewe Mtume, kwa kuyavunja madai yao, “Kwani nyinyi muna ahadi, kutoka kwa Allah Mtukufu, ya jambo hilo? Allah Mtukufu Haendi kinyume ahadi yake. Lakini nyinyi munasema kuhusu Allah Mtukufu msiyoyajua kwa kuzua kwenu urongo.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net