Al-Baqara 2:76
البقرةوَإِذَا لَقُوا۟ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوٓا۟ أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَآجُّوكُم بِهِۦ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Na wanapokutana na wale walioamini, husema: 'Tumeamini.' Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyokufunulieni Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Mola wenu Mlezi? Kwani hamfahamu nyinyi?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo kutana na wale walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyo kufunulieni Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojieni mbele ya Mola wenu Mlezi? Basi hamfahamu nyinyi? [76]
[76] Na kilikuwapo kikundi kingine miongoni mwa wanaafiki wao wakikutana na walio amini husema kwa kuwakhadaa: Tunaamini kuwa nyinyi mnafuata Haki, na kuwa Muhammad ni Nabii aliye tajwa sifa zake katika Taurati. Na wakiwa peke yao na wenzao hulaumiana kwa kughafilika kwa baadhi yao, kwa vile ndimi zao zilivyo teleza katika kuwakhadaa Waumini kuwapa maneno ambayo yatawapa faida makhasimu zao, na wala si lazima katika udanganyifu, wakawatajia yaliyomo katika Taurati ya kueleza kwa sifa kuja kwa Muhammad na kwa hivyo itakuwa hoja juu yao Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa Mayahudi, wakikutana na Waumini, wanasema kwa ndimi zao, “Tumeamini dini yenu na Mtume wenu aliyebashiriwa katika Taurati.” Na wakiwa faragha, wao kwa wao, hawa wanafiki wa kiyahudi, huwa wakiambiana kwa njia ya kukemeana, “Vipi nyinyi mnawahadithia Waumini yale ambayo Allah Mtukufu Amewabainishia katika Taurati kuhusu Muhammad, mkawapa hoja juu yenu mbele ya Mola wenu Siku ya Kiyama? Kwani hamfahamu mkajihadhari?”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net