Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 75

Al-Baqara 2:75

البقرة

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا۟ لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَـٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُۥ مِنۢ بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

Maana

Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wanayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua? [75]

[75] Haikufaliini enyi Waumini kutumai ya kuwa Mayahudi wataiamini Dini yenu na wakufuateni nyinyi, na ilhali katika makundi yao mbali mbali zimekusanyika sifa mbovu zinazo waweka mbali na kuiamini Haki. Walikuwapo baadhi miongoni mwao (nao ni wale Makohani) walio kuwa wakiyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu katika Taurati, na wakiyafahamu vilivyo, kisha makusudi wakiyageuza na hali wanajua kuwa ni kweli, na kuwa vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyo teremshwa haijuzu kuvigeuza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi waislamu! Kwani mumesahau vitendo vya Wana wa Isrãîl, ndipo nafsi zenu zikawa na tamaa kuwa Mayahudi wataiamini dini yenu? Wanavyuoni wao walikuwa wakisikia maneno ya Allah Mtukufu ya Taurati, kisha wakiyapotoa kwa kuyageuza na kuyapa maana yasiyo sahihi baada ya kuyafahamu maana yake ya kweli, au kwa kuyageuza matamshi yake, hali wanajua kuwa wao wanayapotoa maneno ya Allah Mtukufu kwa kusudi na urongo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net