Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 74

Al-Baqara 2:74

البقرة

ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِىَ كَٱلْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ ٱلْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ ٱلْمَآءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ ٱللَّهِ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ

Maana

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayotimbuka mito, na kuna mengine yanayopasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumhofu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika mbali na mnayoyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya. [74]

[74] Tena nyinyi baada ya miujiza na ishara hizi zote hamkukubali wala hamkunyooka, wala nyoyo zenu hazikulainika na kunyenyekea. Bali zikawa zimekacha na ngumu, na zikabakia vile vile na ugumu wake na ushupavu wake, kama jiwe gumu katika ule ukakamavu wake, bali hizo nyoyo zenu zimeshinda jiwe kwa ugumu. Kwani yapo mawe yanayo athirika na kulainika. Yapo mawe yanayo timbuka maji yakawa mito, na yapo mawe yanayo pasuka na yakatoka maji kama chemchem, na yapo mawe kwa uwezo wa Mwenyezi yanayo nyenyekea kufuata mapenzi ya Mwenyezi Mungu yakaporomoka kutoka juu ya milima kama apendavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ama hizo nyoyo zenu,nyinyi Mayahudi, haziathiriki wala hazilainiki. Ole wenu kwa hayo! Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na vitendo vyenu, naye atakupeni adhabu kwa namna mbali mbali za adhabu, ikiwa hamtoshukuru kwa neema mlizo pewa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini nyinyi hamkufaidika na hilo. Kwani baada ya miujiza yote hii yenye kupita mipaka ya uwezo wa kiumbe, nyoyo zenu zilikuwa ngumu kwa namna ambayo hakuna kheri iliopenyeza ndani, na hazikulainika mbele ya miujiza yenye kushinda niliyowaonesha, mpaka nyoyo zenu zikafikia hadi ya kuwa ni kama jiwe gumu, bali zililishinda jiwe kwa ugumu wake. Kwani miongoni mwa mawe kuna yanayopanuka na kutoboka na maji yakabubujika kwa wingi kutoka humo mpaka yakawa ni mito yenye kupita. Na miongoni mwayo kuna yanayofanya nyufa, yakapasuka na kuchimbuka maji ya chemchemi na mikondo. Na miongoni mwayo kuna yanayoanguka kutoka juu ya milima kwa kumwogopa Allah Mtukufu na kumuadhimisha. Na Allah Mtukufu Hakuwa ni Mwenye kughafilika kwa mnayoyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net