Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 77

Al-Baqara 2:77

البقرة

أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ

Maana

Kwani hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyaweka wazi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayo yaficha na wanayo yatangaza? [77]

[77] Hivyo basi haiwapitikii watu hawa na wale kuwa Mwenyezi Mungu hana haja ya kupata hoja kama hizo? Kwani Yeye anajua wanacho kificha na wanacho kidhihirisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, kwani wanafanya uhalifu wote huu na hali wao hawajui kuwa Allah Mtukufu Anayajua yote wanayoyaficha na kuyadhihirisha?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net