Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 7

Al-Baqara 2:7

البقرة

خَتَمَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰٓ أَبْصَـٰرِهِمْ غِشَـٰوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Maana

Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na kusikia kwao, na juu ya kuona kwao kuna pazia. Nao wana adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. [7]

[7] Ukafiri umesaki kwa watu hao, hata imekuwa kama nyoyo zao zimetiwa muhuri, zimezibwa kwa vizibo, haziingii kitu chochote zaidi ya kiliomo ndani yake. Na kama kwamba masikio yao pia yamezibwa, hayasikii onyo lake la kweli, na kama kadhaalika wamefunikwa kwa vitanga vya macho. Hawazioni ishara za Mwenyezi Mungu zenye kuonyesha Imani. Kwa hivyo basi imekuwa wanastahiki kuwafikilia adhabu iliyo kali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu amewapiga muhuri nyoyo zao, masikio yao na ameweka funiko juu ya macho yao ya kuonea kwa sababu ya ukafiri na ujeuri walionao, baada ya haki kuwabainikia. Allah Mtukufu hakuwaafikia kwenye uongofu. Wao watapata adhabu kali katika Moto wa Jahanamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net