Al-Baqara 2:8
البقرةوَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ
Na katika watu, kuna wale wanaosema, "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho", wala wao si Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini. [8]
[8] Na miongoni mwa makafiri wapo watu ambao husema kwa ndimi zao yasiyo kuwamo nyoyoni mwao. Hudhihirisha imani na kusema: "Sisi tunamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama," na wala hawasemi kweli. Basi hao hawaingii katika kundi la Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa watu kuna kundi linalokuwa katika hali ya kutokuwa na uamuzi, linasimama baina ya Waumini na makafiri, nao ni wanafiki wanaosema kwa ndimi zao, “Tumemuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho,’ na hali wao, katika undani wao, ni warongo, hawakuamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net