Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 6

Al-Baqara 2:6

البقرة

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Hakika, wale waliokufuru ni sawa kwao uwaonye au usiwaonye, hawaamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini. [6]

[6] Hii ndiyo hali ya waongofu. Ama wajinga, majaahili, walio acha kujitayarisha kwa Imani kwa mapuuza na kufanya inda, wasimwitikie Mwenyezi Mungu, basi ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walioyakanusha yalioteremshwa kwako kutoka kwa Mola Wako, kwa njia ya kiburi na ujeuri, hakutapatikana kuamini kutoka kwao; ni sawa kwao ukiwa utawatisha na kuwaonya adhabu ya Allah Mtukufu au utaacha kufanya hivyo, kwa sababu wao wameamua kukakamia kwenye njia yao ya batili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net