Al-Baqara 2:5
البقرةأُو۟لَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ
Hao wako kwenye uongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa. [5]
[5] Hawa walio sifiwa kwa sifa zilizo tangulia, wamekua kwa kupata sababu za uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na wamekaa imara juu ya hayo. Wao peke yao ndio walio fuzu watakao pata wayatakayo, na wayatamaniayo, nayo ni malipwa kwa kazi yao na juhudi yao, na kutimiza amri na kuepuka waliyo katazwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wenye sifa hizi wako kwenye nuru inayotoka kwa Mola wao na taufiki inayotoka kwa Muumba Wao na Mwongozi Wao. Wao ndio wenye kufuzu, waliopata matakwa yao na kuokoka na shari ya vitu walivyovikimbia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net