Al-Baqara 2:4
البقرةوَٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ
Na ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako, na Akhera wana yakini nayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo. [4]
[4] Na wale wanao isadiki Qur'ani ulio teremshiwa wewe (Muhammad) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na yote yaliomo ndani yake katika mambo ya hukumu na khabari, na wakatenda yatakikanayo, na wakavisadiki Vitabu vya Mwenyezi Mungu walivyo teremshiwa Manabii na Mitume wa kabla yako, kama Taurati na Injili na vyenginevyo. Kwani risala za Mwenyezi Mungu zote zina asli moja, na hao wanatambulikana kuwa wanaamini Imani moja isiyo legalega ya Siku ya Kiyama na yatayo tokea ya Hisabu na Thawabu na Adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wao ndio ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako, ewe Mtume, ya Qurani, na yalioteremshwa kwako ya hekima, ambayo ni Sunnah, na Vitabu vyote vilivyoteremshwa kwa Mitume kabla yako, kama Taurati, Injil na vinginevyo, na wanaiamini Nyumba ya Maisha baada ya kufa na yaliyomo ndani ya Nyumba hiyo ya kuhesabiwa na kulipwa. Wanaamini hayo kwa nyoyo zao, imani ya kidhati inayodhihiri kwenye ndimi zao na viungo vyao. Kutajwa Siku ya Mwisho mahususi ni kwa sababu kuiamini ni mojawapo ya vitu vikubwa zaidi vyenye kusukuma na kuhimiza kufanya vitendo vya kumtii Allah Mtukufu, kujiepusha na vitendo vya haramu na kuifanyia hesabu nafsi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net