Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 3

Al-Baqara 2:3

البقرة

ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱلْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ يُنفِقُونَ

Maana

Ambao huyaamini ya ghaibu na hudumisha Sala, na hutoa katika yale tuliyowaruzuku.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa. [3]

[3] Na hawa ndio ambao, kwa kuazimia na kunyenyekea, wanayasadiki yale ya ghaibu wasio yaona kwa macho, wala kuyahisi kwa viungo, ambayo ni ya kuitakidiwa na kuaminiwa, kama mambo ya Malaika, Siku ya Akhera. Kwani msingi wa kushika Dini ni kuamini yaliyo ya ghaibu. Pia wakashika Swala vilivyo, kwa kumwelekea Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea kikweli, na wale ambao wanatoa katika yale alio waruzuku Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mambo ya kheri na mema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nao ndio wanao amini ghaibu (ghayb), ambayo haifikiliwi na hisia zao na akili zao pekee, kwa kuwa haijulikani isipokuwa kupitia wahyi wa Allah Mtukufu kwa Mtume wake, rehema za Allah Mtukufu na amani imshukie, kama kuamini Malaika, pepo, moto, na mengineyo katika yale yaliyoelezwa na Mtume Wake, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie yeye. Imani (Ῐmān) ni neno lililokusanya kumkubali Allah Mtukufu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Siku ya Mwisho na Kadari (Qadar), kheri yake na shari yake. Na kutilia nguvu kukubali huko kwa maneno na vitendo, kwa moyo, ulimi na viungo. Na wao, pamoja na kuamini kwao mambo ya ghaibu yasiyoonekana, wanasimamisha Swala kwa kuchunga nyakati zake na kuzitekeleza ipasavyo kulingana na sheria ya Allah Mtukufu kwa Nabii wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye yeye. Kadhalika, katika kile tulichowapa wao, miongoni mwa mali, wanatoa sadaka ya mali zao ya wajibu na ya suna.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net