Al-Baqara 2:2
البقرةذَٰلِكَ ٱلْكِتَـٰبُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka yoyote ndani yake; ni uongofu kwa wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, [2]
[2] Hichi ndicho Kitabu kilicho kamilika, kisicho kuwa na dowa, nacho ni Qur'ani tunayo iteremsha isiyo tiliwa shaka yoyote na kila mwenye akili na mwenye insafu akajua kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wala haitilii shaka kuwa yasemwayo juu ya mambo na hukumu ni ya kweli tupu. Ndani ya Kitabu hichi upo uwongofu ulio kamilika kwa walio kuwa tayari kuitafuta Kweli, na wanajikinga na madhara na mambo ya kuwaletea adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Qurani hii ni kitabu kisicho na shaka kuwa kinatoka kwa Allah Mtukufu. Haifai kwa mtu yoyote kufanya shaka juu yake kwa uwazi wake. Wananufaika kwayo wenye uchajimungu (taqwā), wenye kujikinga kwa elimu yenye manufaa na amali njema, na wao ndio wanaomuogopa Allah Mtukufu na kufuata hukumu Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net