Al-Baqara 2:1
البقرةالٓمٓ
Alif Lam Mim.[1]
[1] Herufi hizi "Alif Lam Mim" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Alif Lam Mim. [1]
[1] Alif Lam Mim: Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ameanzia kwa harufi hizi kuashiria moja katika miujiza ya Qur'ani Tukufu iliyo tungwa kwa harufi zile zile ambazo Waarabu wakitungia maneno yao, na juu ya hivyo wao wameemewa hawakuweza kuleta kitu mfano wa Qur'ani hii. Pia juu ya hivyo hizi harufi zinazindua ili upate kuzingatia yasemwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
“Alif Lam Mim” Herufi hizi na nyinginezo, miongoni mwa herufi zilizotajwa mwanzo wa sura, zinaashiria kuwa Qur’ani haiigiziki. Washirikina waliwekewa ushindani walete kitu kama Qur’ani, wakashindwa kushindana nayo, paomoja na kuwa imejengewa katika herufi hizi hizi ambazo Waarabu wanazitumia. Kulemewa kwa Waarabu kuja na Qur’ani kama hii, ingawa walikuwa ni mafasaha wa watu, ni dalili ya kuwa Qur’ani ni wahyi (waḥy) utokao kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net